IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Nchi za Magharibi zimetenda jinai nyingi pia dhidi ya mataifa

10:02 - January 24, 2019
Habari ID: 3471817
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametilia mkazo kuutazama kila mara kwa jicho baya ushauri wa Wamagharibi, na akafafanua kwa kusema: Nchi za Magharibi, ambazo leo hii zimepata maendeleo mengi katika elimu na sayansi mpya, zimetenda jinai nyingi pia dhidi ya mataifa katika zama zote za historia.

Ayatullah Khamenei, ameyasema hayo Jumatano mjini Tehran katika mkutano na wakuu na watafiti wa Taasisi ya Utambuzi wa Taaluma za Sayansi na Teknolojia (ICSS), Waziri wa Elimu pamoja na wakuu na wahadhiri wa vyuo vikuu husika. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameusia pia kuutumia uwezo na ujuzi wote walionao Wamagharibi kwa ajili ya kupiga hatua kielimu na kisayansi na akasisitiza kwa kusema: Sisi hatuoni aibu kujifunza, bali ni aibu kwetu "kubaki kuwa wanafunzi maisha".

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuhusu ulazima wa kufanywa juhudi za pande zote usiku na mchana ili kuweza kupigwa hatua zaidi katika elimu na sayansi mbali mbali; na akabainisha kwamba: Kasi ya harakati ya kisayansi nchini Iran haipasi kupunguzwa au kusitishwa.

Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa: Taifa lolote linalobaki nyuma katika taaluma mpya na teknolojia zinazohusiana na taaluma hizo halitakuwa na hatima nyingine ghairi ya kubaki nyuma kimaendeleo, kudhalilishwa na kukoloniwa na madola yenye nguvu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, harakati ya kisayansi nchini Iran imepiga hatua nzuri katika kipindi cha miaka 20 ya karibuni, lakini akasisitiza kwamba: Kasi ya harakati hii haipasi kupungua, bali inapasa idumishwe na kuimarishwa kwa miaka 20 hadi 30 ijayo mpaka tufikie nukta ya kileleni.

Ayatullah Khamenei ameashiria pia mifano ya kihistoria katika baadhi ya nchi ambazo zilijiwekea misingi ya maendeleo ya kielimu na kisayansi katika mazingira magumu kabisa, na akaongezea kwa kusema: Mazingira tuliyonayo sisi hii leo hayafikii ugumu wa mitikisiko iliyokuwepo katika nchi hizo, kwa hivyo tunao uwezo wa kujijengea misingi imara ya kielimu.

3783796

captcha