IQNA

Israel imeua Wapalestina zaidi ya 254 na kujeruhi wengine 23,000 Gaza

9:17 - January 23, 2019
Habari ID: 3471816
TEHRAN (IQNA)- Jeshi la utawala haramu wa Israel limeua zaidi ya Wapalestina 254 na kuwajeruhi wengine wasiopungua 23,000 tokea yaanze 'Maandamano Makubwa ya Haki ya Kurejea' ambayo yalianza kufanyika kila Ijumaa kuanzia Machi 30 mwaka 2018.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotangazwa Jumatatu na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, tokea Machi 30 2018, Ukanda wa Ghaza umeshuhudia ongezeko kubwa la Wapalestina wanaouawa katika maadanmano katika eneo linaloteganisha utawala wa Israel na Ukanda wa Ghaza. OCHA imethibitisha kuwa, Jeshi la Israel limeua Wapalestina 254 katika Ukanda wa Ghaza tokea Machi 30 hadi Disemba 31 mwaka 2018. Ripoti hiyo imesema 180 miongoni mwao wameuawa katika Maandamano Makubwa ya Haki ya Kurejea na matukio yanayohusiana na maandamano hayo. Aidha taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa imesema miongoni mwa Wapalestina hao waliouawa kwa risasi za jeshi katili la Israel, 44 walikuwa ni watoto na wanne ni wanawake.

Tangu tarehe 30 Machi mwaka huu hadi hivi sasa, Wapalestina 247 wameshauawa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi makatili wa Israel na zaidi ya 25 elfu wengine wameshajeruhiwa.

Nchi nyingi duniani ikiwemo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na mashirika mbalimbali ya kimataifa, yamekuwa muda wote yakilaani jinai zinazofanywa na Wazayuni dhidi ya Wapalestina.

Wimbi hili la maandamano ya Wapalestina ni la kukumbuka jinai nyingine ya utawala wa Kizayuni ya kuteka ardhi nyingine za Wapalestina tarehe 30 Machi 1976.

Siasa kuu za utawala wa Kizayuni wa Israel ni kuwapora Wapalestina ardhi zao na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kwa shabaha ya kuvuruga muundo wa kijiografia wa maeneo ya Palestina na kuyapa maeneo hayo sura ya Kizayuni.

3467758

captcha