Jumuiya ya Kiislamu ya Miami Valley jimboni Ohio imesema imeanzisha mkakati wake kwa kuwafunza wakaazi wa mtaa wa Springfield kuhusu mafundisho sahihi ya Uislamu.
Hafla hiyo imepangwa kufanyika Jumamosi Oktoba 13 katika Ukumbzi wa Bayley katika Chuo Kikuu cha Wittenburg na watu wote wamakaribishwa kuhudhuria.
Siku ya Kiislamu Ohio imekuwa ikifanyika katika Jumamosi ya pili mwezi Oktoba kwa miaka 31 kabla ya kusimamishwa mwaka 1997 kutokana na kuenea chuki dhidi ya Uislamu. Mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 yalishadidisha zaidi vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu nchini Marekani.