IQNA

Nakala 20,000 za Qur'ani Kusambazwa Amerika ya Latini

12:37 - February 12, 2018
Habari ID: 3471388
TEHRAN (IQNA)-Taasisi ya Masuala ya Kidini –Diyanet- ya Uturuki (TDV) imetoa zawadi ya nakala 20,000 za Qur'ani Tukufu ziliotarujumiwa kwa Kihispania kwa ajili ya kusambazwa katika nchi za Amerika ya Latini.

Katika taarifa, Taasisi ya Diyanet imesema nakala hizo za Qur'ani zitasambazwa miongoni mwa jamii za Waislamu katika nchi za Guatemala, El Salvador, Colombia, Haiti, Argentina, Chile, Peru, Bolivia, Ecuador na Uruguay. Nakala hizo za Qur'ani ambazo zina lugha mbili za Kihispania na Kiarabu zinasambazwa zinasambazwa katika kampeni ya, "Zawadi yangu ni Qur'ani."

Taasisi ya Diyanet inasema kampeni hiyo ilianzishwa kwa lengo la kukidhi mahitaji ya Waislamu wengi duniani na kwamba hadi sasa nakala milioni moja za Qur'ani zimesambazwa katika nchi mbali mbali.

Ilyas Serenli, naibu mkuu wa bodi ya Taasisi ya Diyanet amesema hivi sasa wako mbioni kutayarisha tarjama ya Qur'ani kwa lugha ya Kireno kwa jili ya Waislamu wa Brazil.

Taasisi ya Diyanet ina mradi wa kutayarisha tarjama za Qur'ani kwa ligha kadhaa na hadi sasa wamefanikiwa kuchapisha tarjama za lugha 17.

3465164

captcha