Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wanafunzi waliojisajidi ni kutoka shule za umma na pia shule binafsi katika nchi hiyo ndogo ya Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi.
Mashindano hayo yameandaliwa Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kiislamu Qatar kwa ushirikiano na wizara ya elimu nchini humo. Usajili wa washiriki wa mashindano hayo ulianza kati kati ya mwezi Oktoba na utaendelea hadi Februari 11.
Wanaoandaa mashindano hayo wametoa wito kwa wanafunzi waendelee kujisajili kwa ajili ya mashindano hayo ambayo yatafanyika baadaye mjini Februari mwakani.